Showing posts with label mastaa. Show all posts
Showing posts with label mastaa. Show all posts

MASTAA WENGINE WAFUNGUKA KUHUSU KIFO CHA MANDELA.....

TWEET ZA WANAMUZIKI WA NJE BAADA YA KIFO CHA NELSON MANDELA....

Mwanamuziki Robert Sylvester Kelly "R. Kelly" akiwa na Nelson Mandela enzi za uhai wake.
 

UTENGENEZAJI WA FAST AND FURIOUS 7 KUENDELEA BAADA YA KUSIMAMA KWA MUDA KUTOKANA NA KIFO CHA MMOJA WA MASTAA WAKE,PAUL WALKER....


Paul walker enzi za uhai wake

Utengenezaji wa filamu mpya ya Fast and Furious utaendelea licha ya kifo cha mmoja wa mastaa wake, Paul Walker. Utengenezaji wa filamu hiyo yenye bajeti kubwa ulikuwa umesimama weekend wakati wa sikukuu ya Thanksgiving ambapo Walker alipata ajali na kufa siku ya Jumamosi. Walker alikuwa arejee kuendelea na utengenezaji wa filamu hiyo jijini Atlanta nakuungana na mastaa wenzie Vin Deisel na Dwayne Johnson aka The Rock. James Wan, ambaye ni muongozaji wa filamu hiyo na wakurugenzi kutoka Universal Studios walifanya mkutano jana asubuhi kujadili jinsi ya kuendelea na Fast and Furious 7 katika njia ambayo itakuwa na heshima kwa kifo cha Walker. Kwa mujibu wa The Hollywood Reporter, kushoot kunaweza kuanza Jumanne hii. Walker alikuwa akiigiza kama Brian O'Conner, mhalifu aliyebadilika na kuwa polisi kwenye Fast and Furious 7, uhusika alioucheza katika filamu sita zilizopita za Fast and Furious. Shooting ya filamu hiyo itamalizka Januariy huko Abu Dhabi.
Fast and Furious 7 ilipangwa kutoka July 11, 2014.

PICHA ZINATISHA! MWILI WA MAREHEMU PAUL WALKER WA FAST AND FURIOUS WAONYESHWA....

.Paul Walker
Paul WalkerKwa mara ya kwanza mwili wa marehemu Paul Walker wa Fast 5 and Fast & Furious 6 umeonyeshwa kwa ulivyoonekana hapo juu

PICHA: HATIMAYE MWANAUME MREFU KULIKO WOTE DUNIANI APATA MKE.....
RIHANNA APIGA PICHA ZA UCHI KWA AJILI YA JARIDA LA GQ UINGEREZA


KAMA kawaida yake, Rihanna amepiga picha kwa ajili ya jarida la GQ la Uingereza akiwa nusu utupu tangu juu hadi chini. 
 
Mwimbaji huyo maarufu duniani amelipamba jalada la mbele la jarida hilo toleo la Novemba akiwa hajavaa chochote cha maana tangu juu ukiachilia mbali kichwa chake ambacho kimezingirwa na kufunikwa na majoka.

Picha hizo zimepigwa na Mariano Vivanco kwa kusimamiwa na Damien Hirst, zikitoa taswira ya simulizi ya Kigiriki kuhusu Medusa (mlinzi wa kike) ambayo imetumika katika kuadhimisha mwaka wa 25 wa jarida hilo. 
 
Toleo hilo litakuwa mitaani tarehe 31 Oktoba mwaka huu.

Bofya  hapo  chini  kuziona  picha  zake....

<< BOFYA  HAPA  KUONA  PICHA>>
 

NANDO ACHAGULIWA KURUDI TENA MJENGONI KUIWAKILISHA TANZANIA KWENYE BIG BROTHER MWAKANI.....Ammy Nando ambaye alituwakilisha mwaka huu katika shindano la Big Brother Africa, The Chase amepata nafasi ya kutuwakilisha tena katika shindano hilo hapo mwakani 2014. Taarifa kutoka vyanzo vya kuaminika katika Ofisi za Multi Choice Tanzania zimethibitisha hilo. Nando alikuwa disqualified na kutolewa katika shindano hilo mwaka huu baada ya kugombana na kutishia kumchoma kisu mshiriki kutoka Ghana anayejulikana kama Elikem. Sasa sijui jamaa kajirekebisha na hataleta fujo tena???? Habari za uhakika zinathibitisha kuwa Nando amekubali ofa hiyo na yuko tayari kwenda kuipeperusha bendera ya Tanzania tena.......

PICHA ZA UCHI ZA KIM KARDASHIAN ZAWAKWAZA MASHABIKI WAKE....
TV star Kim Kardashian ambae ni baby mama wa rapper Kanye West ameingia tena kwenye headlines baada ya picha zake kusambaa akiwa ameziba tu sehemu ndogo ya mwili wake huku akiweka msisitizo kwenye instagram kwamba #Nofilter yani hajaongeza mbwembwe zozote za kiteknolojia kwenye muonekano wa picha.
 
Kanye West alipoiona hiyo post aliiRETWEET na kuandika ‘naelekea home now’ ambapo kwa fans walioziona picha hizi kila mmoja kaandika la kwake ila amepata lawama nyingi za kushindwa kujiheshimu na kutambua kwamba yeye ni Mama wa mtoto mmoja sasa hivi.

<<PICHA  YA  KWANZA >>

<< PICHA  YA  PILI >> 

Bofya  hapo  juu  kujionea  picha  hizo

DAVIDO WA NIGERIA KUTUMBUIZA KATIKA FAINALI ZA SERENGETI FIESTA JIJINI DAR WIKI IJAYO,PATAKUWA HAPATOSHI.....!!


Homa ya tukio kubwa la burudani ambalo hufanyika kila mwaka inazidi kupanda, of course naizungumzia Serengeti Fiesta 2013 ambayo baada ya kuzunguka mikoani na kuacha historia sasa mashambulizi yamehamia katika fainali inayotarajiwa kufanyika wiki ijayo jijini Dar es salaam.
 
Kila mmoja bado anajitahidi kubashiri ni wasanii gani wa kimataifa watakaoshambulia jukwaa hilo mwaka huu, lakini mmoja wao amewekwa hadharani jana (October 17) kupitia XXL ya Clouds FM naye si mwingine bali ni Dami Duro hit maker Davido.
 
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Davido kuperform Tanzania katika jukwaa la Fiesta hivyo inatoa picha ni kiasi gani patakuwa hapatoshi pale viwanja vya Leaders Jumamosi ijayo (Oct 26) katika fainali ya Serengeti Fiesta 2013.
 
Davido  ni  nani?
Jina lake kamili ni David Adedeji Adeleke aka Davido kutoka Nigeria. Ni mmoja kati ya wasanii wakubwa wa Africa na anatokea katika familia ya mfanya biashara bilionea aitwaye Dr Deji Adelek.

Davido ambaye mwezi November atatizmiza miaka 21 alizaliwa Atlanta, Georgia Marekani Novemba 21, 1992 na kukulia Lagos, Nigeria.
 
Alianza kuonekana kwenye spotlight mwaka 2011 kupitia wimbo wake maarufu ‘Back When’ aliomshirikisha star mwingine wa Nigeria Naeto C.
 
Mbali na kuimba Davido pia ni mwandishi wa nyimbo na producer na anamiliki Record label yake inayoitwa HKN Music.
 
Mbali na muziki Davido pia ni mwanafunzi wa chuo cha Babcock huko Nigeria akichukua Business Administration.
Kati ya Hit Songs za Davido ambazo bila shaka ataziperform live katika Serengeti Fiesta Jumamosi ijayo ni pamoja na Dami Duro, Back when, Gobe, na Zingine

 
-Kwa hisani ya Bongo5

MWIGIZAJI MAARUFU VAN VICKER ASHEREKEA MIAKA 10 YA NDOA YAKE...Juzi,october 16th ilikuwa ni siku ambayo Van Vicker na mke wake wamefikisha miaka kumi tangu waoane. Mwigizaji Van Vicker ameonyesha picha ya zamani ya mwaka 1995 ya yeye na mke wake. Ni miaka 19 sasa tangu waanze  mahusiano. Mastaa wengi imekuwa tabu kumaliza hata mwaka kwenye mahusiano,sijui wanakuwa na matatizo gani lakini hawa kweli ni mfano wa kuigwa kwasababu ukiacha dunia hii iliyoharibika wameweza kudumu kwa miaka 19 kwenye mahusiano na tangu waoane ndoa yao imekuwa imara mwaka wa kumi sasa. Kwanza nawapongeza alafu naiombea familia yao maisha marefu yenye upendo kama huo na kuwaasa mastaa wengine kuiga mfano huu kuacha au kuachwa mara kwa mara sio sifa nzuri. Wao kama vioo vya jamii inawabidi kutuonyesha sisi mambo mazuri ya kuiga na sio skendo kila iitwapo leo....


Kuonyesha furaha yake Van Vicker aliandika ujumbe ufuatao


PICHA: ASHANTI ASHEREKEA BIRTHDAY YAKE, AMEFIKISHA MIAKA 33....

Msanii aliyekuwa chini ya record lebel kubwa duniani 'Murder Inc' amesherekea siku yake ya kuzaliwa na marafiki wake wa karibu weekend hii. Ashanti amefikisha miaka 33 na mara ya mwisho amezungumza kuhusu muziki wake alisema hajafeli baada ya kutengana na Murder Inc ila ana fanya bidii za kurudi na solo project, anacho hitaji ni muda.

Mwezi ujao November 9 anatoa album yake mpya na ya tano inayoitwa 'BraveHeart' .


 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter